Leteni zaka kamili katika nyumba yangu ili kiwemo chakula katika nyumba yangu,mkanijaribu kwa njia hiyo,asema Bwana wa majeshi, mjue kama sitawafungulia madilisha ya Mbinguni na kuwamwagieni baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha.
Nami kwaajili yenu nitamkemea Yeye alaye wala hatapuktisha mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba asema Bwana wa majeshi.Na matfaifa yote watawiteni heri.Maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana asema Bwana.
Mungu amesema nijaribuni kwa njia hiyo muone.
Kuna wakati wowote Mungu amesema nijaribuni katika maandiko ipo kwenye malaki pekee kwamba anataka ajaribiwe hapo wala si pengine Mungu huwezi ukamjaribu kwa njia yoyote ile isipokuwa katika Fungu la Kumi za sadaka mbalimbali.Ziko baraka zitokanazo na Fungu la kumi nakwambia ukiwa mwaminifu Mungu hawezi akakuacha atafanya yeye si mwongo.
BARAKA ZITOKAZO NA FUNGU LA KUMI
- Fungu la kumi linaachilia mipenyo. ( Mjue kama sitawafungulia madilisha ya mbinguni)
Kama vile dilisha lipitishavyo(lipenyeshavyo) mwanga ndivyo utakavyo kuwa wewe.Anaposema dilisha anazungumzia mahali mtu anapatia kitega uchumi chako. Kila unapotoa Fungu la Kumi Mungu anatengeneza vitega uchumi vipya vya kuleta baraka kwako. madilisha ni vipitishi chanzo cha mapato ya mtu ukiona mtu yupo ndani ya kanisa hana kazi di dhahili kwamba siyo mwaminifu katika fungu la kumi maana ukiwa unatoa fungu la kumi Mungu anashughulikia madilisha yaani mahali pa kupatia, anahakikisha kama huna kazi anapata kazi.
2.Kujazwa.
Nakuwamwagieni baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha.
Hii ni baraka ya pili ya fungu la kumi kila utoapo fungu la kumi Mungu anakujaza hata kama ulikuwa nacho kidogo Mungu anakiongeza ili kiwe kikubwa.Kila utowapo fungu la kumi kuna hatua unapiga kiuchumi huwezi ukawa palepale. Wewe andaa tu ghala zako tena zisiwe ndogo maana ipo siri ya ajabu hapa kila utoapo fungu la kumi, anasema nitakumwagia baraka mtu anapotaka kumwaga kitu anatumia nguvu, Mungu anapokumwagia baraka antumia nguvu hata isiwepo nafasi ya kutosha. Unabarikiwa hadi unakosa kwa viweka hiyo ni siri ya Fungu la kumi.
3.Linamfanya Mungu awe na hasira juu ya walao.
Nami kwaajili yenu nitamkememea yeye alaye.
4.Linampa Mungu hasira kali juu yao waharibo.
Wala hataharibu mazao ya ardhi yenu.
Je unataka kuona Mungu akiingia vitani juu ya roho za uchawi katika mali zako toa fungu la kumi.Anasema wala hata haribu mazao ya ardhi yenu. Kila ulicho tolea fungu la kumi wachawi wala shetani akigusi akigusa kinamuunguza ni cha moto.
Kuna watu wanatumwa kufanya uharubifu kwaajili ya mali zako mifugo yako mazao ya arthi yako je unataka uwe tishio kwao toa fungu la kumi utaona utetezi wa kimungu. Kila utoapo fungu la kumi unamfanya Mungu avae sura ya ukali kwa waharibifu wa mali zako.
5. Mafaikio ya kudumu.
Wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba yenu.
Kila baraka inayoingia kwenye maisha yake ina wakati wake wa kuisha. na ndiyo maana ipo misimu katiaka maisha fungu la kumi linasababisha kitu kiishe kwa wakati.tatizo kubwa ukiona pesa ya kuisha mwezi mzima imekaa siku kumi ujue unatembea kwenya laana itikanayo na kutokutoa Fungu la kumi.mpo watu wachache lakini chakula kinaisha kabla ya wakati mnakula kidogo tu lakini vinaisha sana kama hutoifungu la kumi ipo huwezi ukawa na vitu vya kudumu vitakuwa vinapukuchika siku mapaka siku.Mtu atoaye fungu la kumi anabaraka ya kuvifanya vitu vyake visipukuchike.Kuisha kabla ya wakati kwa lugha nyingine ni kufirisika, kila mtu atashangaa
6.Kubadilishwa jina.
Mataifa yote wata waiteni heri.
Kazi ya fungu la kumi ni kukubadilishia majina uliyo nayo lenyewe linafuta kabisa majina yasiyo yautukufu wanayokita watu.Tunajua ipo nguvu ndani ya majina.Kuna wakati fulani mtu aliniita tapeli, siku hiyo nilichkia sana kwa yule mtu kuniita hivyo, nikajiuliza kwanini huyu mtu aniite mimi tapeli ? nimewahi kutapeli nini kumbe sikuwa mwaminifu katika mafungu ya kumi usipokwa mtoaji wa mafungu ya kumi Mungu atakuwa anawaambia watu mwite tapeli wewe.Mungu aliwaita wana waisraeli waizi kwasababu ya kula mafungu ya kumi kwa kuwa Mungu hakuamini hata watu hawatakuamini, utoapofungu la kumi jiandae kuitwa heri yaani baraka hata kama hujasoma watasema msomi,hata kama mfanyakazi wakawaida watasema meneja, hata kama hata kam huna watakupa maana Mungu atawaaminisha kwamba wewe ni chanzo cha baraka
7.Kubadilishwa mwonekano.
Utakuwa nchi ya kupendeza sana asema Bwana wa majeshi.
Ubarikiwe wewe uliyesoma nakujifunza tendea kazi utauona mkono wa Bwana
Kwa mawasiliano
vodacom 0764901546.
Email: adstep4@gmail.com
Changizo kwaajili ya huduma kupitia M-pesa namba 0764901546 kutoa ni moyo na si utajiri.
Kila usomapo ujumbe huu coment.
Baraka saba za Fungu la kumi
Reviewed by adam
on
Januari 17, 2017
Rating:
Hakuna maoni: