Unapongezwa kwa kuwa umefanya uamuzi wa busara, umechukua hatua ambayo haitokufanya ujute maishani mwako, endelea kufurahia maisha mapya ndani ya Yesu.
Wakati mimi naokoka walitokea watu walionihesabia siku, kwamba waone kama ndaendelea na wokovu, walihesabu siku mpaka sasa wamechoka kuzihesabu, na wewe pia usihofu watatokea wengi watakatakukatisha tamaa,watakao kuhesabia siku itafika tu wakati watakata tamaa kwa ajili yako.
Yohana 10:27-28.
Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua nao wanifuata.Nami nawapa uzima wa milele wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakaye wapokonya kwenye mkono wangu.
Ahadi ya Yesu ni hii kwakuwa umekubali umesikia sauti yake na kumfuata hakuna mtu atakaye kutoa kwenye mkono wake.
Watatokea wengi marafiki, ndugu, mume, mke, viongozi wa serekali, wazazi ili wakutoe kwenye mkono wa Yesu, Yesu anakuhakikishia usalama wa maisha yako sasa kwamba upo mkononi mwake, hakuna atakaye weza kukutoa kwenye mkono wake.
Wakati mimi naokoka wazazi wangu walikuja kinyume na kuokoka kwangu, nilishangaa sana, nikakuta chuki tu ya ghafla, wakisema kwanini, umeokoka umetuletea kitu kipya katika familia yetu, sisi dini yetu hairuhusu mtu kuokoka, pamoja na kwamba walisema, mimi nilikaza msimamo kwamba nimeamua kuokoka sitorudi nyuma, wazazi wangu walisimama kufanya fujo, wakanifukuza nyumbani wakasema kwa kuwa umeokoka hatutaki tukuone hapa nyumbani, wala kulala, wala kula wala kuja kutuomba chochote kinachohusu shule yako.
Mimi bado nilikaza msimamo nikaondoka nyumbani, Yesu anasema wala hakuna mtu atakaye kutoa kwenye mkono wangu, wakati huo nilikuwa bado mtoto mdogo sana, nikaelekea kwa mchungaji nikwamwambia yote yaliyotendeka, wakati wao walinikana eti kwasababu nimeokoka Mungu akaniinulia wazazi wengine, wakasema kwanzia sasa utalala, wakanipa na chakula, na nilipohitaji mahitaji ya shule walinipatia, kwa muda.
Yesu anakupa uhakika kwamba upo kwenye mkono salama, hata kama leo rafiki zako watakutenga, Yesu yeye ni rafiki yako, atatembea na wewe, hata kama ni wazazi ,Yesu atakupa wazazi wengine, hata kama ni mume au mke usihofu upo kwenye mkono salama.
Ndiyo maana unapewa pongezi, kwa kuwa umechagua fungu jema lakutembea na Yesu
MAMBO YALIYOTOKEA BAADA TU YAKUOKOKA
Ukweli ni kwamba hakuna mtu apitaye katikati ya moshi, halafu harufu ya moshi isibaki katika nguo zake, na hakuna mtu aliyeokoka asione mabadiliko ndani ya Yesu. Yapo mabadiliko yanayotokea baada tu yakuokoka najua unapenda ujue nikinini kimekupata baada yakumpokea Yesu.
1.Umekuwa kiumbe kipya.
Kuwa kiumbe kipya ni kuanza maisha mapya ndani ya Yesu, maisha ya zamani yaani maisha ya kale, yamepita, Mungu anakufannya upya fahamu zako, mitazamo yako, njia zako, tabia zako, mwonekano wako, ongea yako na tembea yako.
Yote ndani ya Yesu yamekuwa mapya, hili ndilo lililo kutokea baada tu yakuokoka, Mungu hanakumbukumbu zako za nyuma ameanza na wewe upya bila kuangalia juzi ulifanya kitu gani.
2 wakorintho 5:17
Hata imekuwa. mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! yamekuwa mapya.
Shetani wala mtu wa aina yeyote asikwambie mambo ya kale, mambo ya kale ni mambo yaliyokwisha kupita, mtu asikwambie jana nilikuona unazini, mtu asikwambie jana nilikuona unavuta siganara na kunywa pombe, hayo ni mambo ya kale, ambayo hujaingia nayo ndani ya Yesu, akiwapo mtu yeyote atakayekwambia hayo mwambie kwamba.
mtu akiwapo ndani ya Yesu amekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya.
2.Umekuwa mtoto wa Mungu.
Wewe sasa ni mtoto wa Mungu, Mungu ni Baba yako, kabla hujaokoka ulikuwa mtu tu mbele za Mungu, kwasababu tu uliumbwa na Mungu, ila baada ya kumpokea Yesu yapo mabadiliko ambayo yametokea, umekuwa mtoto wa Mungu.
Yohana 1:12
Bali wate waliompokea aliwapa uwezo wakufanyika watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake.
Ni furaha iliyoje kuwa mtoto wa Mungu, Mungu anataka uringe kwakumpokea Yesu, maana sasa Mungu hakutazami tena kama adui bali kama mtoto wake, wewe ndiye prince mbele za Mungu, maana Mungu ni mfalme wetu.
Kwanzia sasa ona ulichopokea nicha thamani hata uitwe mtoto wa Mungu.
3.Umepita kutoka mautini na kingia uzimani.
Hapo ulipo, wewe ni wauzima, ulipompokea Yesu tu umepita kutoka mautini na kuingia uzimani
Yohana 5:24
Amini, amini nawaambia yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
Kabla ya kuokoka ulikuwa kwenye mauti, Yesu amefanyika daraja lakukuvusha kutoka mautini na kuingia uzimani sasa unao uzima wa milele ndani yako kwa tendo tu la dakika chache ambalo umekubali kulitenda.
4.Unalindwa na malaika wa Mungu.
Mungu amekuwekea ulinzi wa kutosha kwenye maisha yako, baada tu yakuokoka unalo kundi kubwa la malaika wanaokulinda, ukiokoka hata wachawi wanakuogopa maana wanapotafuta kukushambulia malaika za Mungu wanapigana upande wako, huna haja ya kuogopa tena.
Waebrania 1:14.
Je! hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumia wale wote watakao urtithi wakovu?.
Hao roho wanaotumwa kwaajili yako ni malaika atayerithi wokovu ni wewe, hivyo kila unapotembea kwanzia sasa hauko peke yako, hata chumbani kwako hata kama humwoni mtu, ila malaika wa Mungu wanakuwa na wewe.
Zaburi 34:7
Malaika wa Bwana hufanya kituo.Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa
Wewe umekuwa kituo cha malaika, malaika wakikuona wewe wanatua kukulinda, baada ya kuokoka hutoona tena kukabwa na wachawi, maana malaika wanakupigania sana. Zamani ulikuwa ukitumia hirizi, ili kujikinga lakini sasa hauhitaji tena mganga wa kienyeji ili akuchanje chale katika mwili wako inatosha tu hao malaika wanapambana na nguvu yoyote inayosimama kinyume na mipango ya Mungu katika maisha yako.
5.Umepewa mamlaka dhidi ya nguvu za giza.
mfano mzuri wa mamlaka ni kwa trafiki aliyepo barabani, anaweza akawa mwembamba sana, na gari kubwa kama skania ikawa inapita, trafiki akinyosha mkono tu, skania inasimamishwa. Kwanini raia wengine hawawezi ila trafiki tu, ni kwasababu ya mamlaka. Sasa baada tu yakuokoka Mungu amekuvisha mamlaka juu ya nguvu za giza kama vile wachawi, waganga, mapepo, majini, shetani na ...nk
Luka 10:19
Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui wala hakuna kitu kitakacho wadhuru.
Ni wakati wa kutumia mamlaka yako, maana hiyo ni zawadi baada yakumpokea Yesu, Mungu anakukabithi mamlaka, kwasababu wewe kama mtoto wa Mungu hautakiwi uonewe, kabla hujaokoka wachawi, walikuwa wanatembea kwenye mwili wako, nyumba unayo kaa ni nzito, lakini sasa unaweza ukasimama ukasema kwa jina la Yesu Kristo nakanyaga uchawi na kuondosha katika maisha yangu na ikawa.
6.Jina lako limeandikwa mbinguni kwenye kitabu cha uzima.
Siku moja Yesu aliwatuma wanafunzi wake wakawafanyie watu maombezi, siku hiyo ilikuwa ni siku ya furaha kwa wanafunzi wake, wakarudi na taarifa kwamba Bwana hata pepo wanatutii kwa jina lako. Yesu akawajibu akawaambia msifurahi kwa vile pepo wanawatii bali furahini kwasababu majina yenu yameandikwa mbinguni.
Ndugu mpendwa uliyempokea Yesu, ule wakati tu ulipoongozwa sala ya toba, tendo kubwa lilifanyika mbinguni, na tendo hilo ni kwamba jina lako limefutwa kabisa kwenye kitabu cha hukumu na kuandikwa kwenye kitabu cha uzima.
Kipo kitabu cha uzima na kitabu cha hukumu, kitabu cha uzima ni kitabu ambacho kinamajina ya wote waliokoka, na kitabu cha hukumu ni kitabu ambacho kimeandikwa majina yote ya watu wasiookoka, ambao hawa kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yao wakiwa duniani.
kutoka 32:32-33
Lakini sasa, nakusihi wasamehe dhambi yao, lakini kama sivyo, basi nifute kutoka kwenye kitabu ulichoandika.BWANA akamjibu Musa, “Ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta kutoka kwenye kitabu changu.
Luka 10:20
Lakini msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii, bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.”
Ufunuo 20:15
Na iwapo mtu jina lake halikuonekana katika kile kitabu cha uzima, alitupwa ndani ya lile ziwa la moto.
HAKIKA YA WOKOVU WAKO
Mwengine anakuwa hana uhakika na wokovu wake anajihisi, labda sijasamehewa, maana anaangalia mambo aliyokuwa anatenda kipindi bado hajamkabithi Yesu maisha yake.Ukweli ni kwamba umesamehewa wala nafsi yako au mtu awaye yeyote yule asikuhukumu.
Shahidi wa kwanza anayejua kwamba wewe umesamehewa dhambi ni neno la Mungu, shahidi si yule aliyekuona wakati unapomkiri Yesu na kuungama dhambi zako, shahidi wa kweli na asiye shakiwa ni neno la Mungu, Je! neno la Mungu linasemaje kwa wewe uliyetubu dhambi na kumpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako.
Isaya 44:22
Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito, dhambi zako kama wingu. Nirudie maana nimekukomboa.
Neno la Mungu ndiyo katiba inayotupa uhakika ya kwamba umesamehewa, Mungu amefuta makosa yako, amesafisha kabisa uovu wako haijarishi huo uovu, ulikuwa wa namna gani, mwingine anaweza akawaza mimi niliyetoa mimba na mimi nimesamehewa ? ukweli ni kwamba hata dhambi yako ingekuwa nzito sana kama wingu zito la mvua, na kama wingu zito la mvua linavyoondolewa katika anga ndivyo ambavyo Mungu ameuondoa uovu wako.
Isaya 1:18
Haya, njoni tusemezane asema Bwana.Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana zitakuwa njeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera zitakuwa kama sufu.
Yeremia 33:8
Nami nitawasafisha na uovu wao wote ambao kwa huo wamenitenda dhambi na kukosa juu yangu.
Haina haja tena ya kuwa na mashaka na kusamehewa kwako shahidi wako wakusimama naye ni neno la Mungu, yeye amekuhakikishia kwamba dhambi zako hazikumbukwi maana Mungu amezifuta hazipo,usijihukumu, jisamehe mwenyewe maana Mungu amekusamehe
Isaya 43:25
Mimi naam mimi, ndimi nizifutaye dhambi zako, kwa ajili yangu mwenyewe,
wala sizikumbuki dhambi zako tena.
Mungu anaongea kwamba yeye hakumbuki dhambi zako baada tu ya kutubu na kumkubali Yesu kama Bwana na mwokozi wa misha yako, chochote kwenye maisha yako kinachokukumbusha kwamba wewe kumbuka ulizini, ujua ni shetani hataki aone ukiendelea na wokovu wako, usikubali wala kusikiliza maana wewe umeokoka na Yesu yupo pamoja na wewe.
HONGERA KWA KUOKOKA
Reviewed by adam
on
Machi 22, 2017
Rating:
![HONGERA KWA KUOKOKA](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7cUXclZvhzuQFjh3Q-7F2Hr4TRHyA5kKkeGJYJ51j_DU4RcNGS4-J5PPTbmenUssGoQNEMEZ0_aTryYxqQmq-oomvpC57cTsdfX8hZT6WY1WrCDlWcQffyBhM0tt54_J8miGXNCkAI1Ux/s72-c/index.png)
Hakuna maoni: