MTU WA MALENGO
Lengo ni shabaha ya kufanya jambo fulani, au ni kusudio la
kufanya kitu fulani,au wazo fulani linalokupeleka mahali fulani.
mtu wa malengo ni mtu
anayefanya kitu kwa shabaha.
Binadamu ni kiumbe cha malengo, ili ujitofautishe na wanyama
ni lazima uwe kiumbe cha malengo, ukikosa malengo wewe ni sawa sawa na mnyama
tu ndivyo Mungu anavyokuona na ndivyo ulivyo.
Mithali 18:3
Mkabithi Bwana kazi zako,
Na mawazo yako yatathibitika.
Mawazo ni makudio, mawazo ni malengo, mawazo ni shabaha,
mawazo ni mipango, kila jambo analolifanya mtu linaanzia kwenye mawazo liwe
jambo baya au jema.
Kazi yetu ni kuwaza, kazi ya Mungu ni kudhibitisha mawazo
yetu, ukikosa malengo utakuwa sawasawa na mwindaji anapiga ndege bila kupima
kwanza, malengo ndiyo kipimo chako.
KWANINI TUWEKE MALENGO.
Tunapimautendaji kwa kuweka malengo, ni sawa sawa na
mwanafunzi aliyeweka malengo yakupata A, anajipima kwa kupitia lengo halafu
akapata B maana yake amefeli kwasababu hajapata A aliyoilenga, au mtu
anayefanya buashara katika bidii yake yote alipanga apate 10000 kwa kila siku
siku akipata 5000 kwa siku atajua amefeli, malengo ndiyo kitu cha kulinganisha.
Huwezi ukajua mwisho wa safari yako kama huna malengo, mtu
asiyekuwa na malengo ni sawa na mtu ambaye anasafiri ila hajui mwisho wa safari
yake, hata magari yanayosafirisha abilia yanaandikwa Mbeya hadi Dar -es –salam,
mtu akifika Iringa anajua kwamba bado hajafika, akifika Morogoro anajua bado
hajafika, asiye na malengo anaweza akashuka hata mahali siyo mwisho wa safari
yake. Siku moja nilimwuliza mtoto wa shule nilipokuwa nikifundisha somohili
kanisani nikamwambia ukimaliza shule unataka kuja kuwa nani? Akaniambia nataka
kujakuwa Rubani, anasoma ila anajua mwisho wa safari yangu ni kuwa Rubani,
unafanya biashara mwisho wa safari yako ni kuwa nani?, unasoma mwisho wa safari
yako ya kisomo ni kuwa nani, kama hujajua utakatisha masoma, au utasoma kupita
kiasi.
Katika vitu ambavyo watu wamefeli, nikutokutunza muda, na
sababu ni kukosa malengo, ukikosa malengo utashindwa kutunza muda,ukiwa na malengo
muda utakuwa dhahabu kwako, maana kina punzi ya uhai unayoivuta itakuwa ni
faida kwako.Zamani walikuwa wanakamata uzululaji, kuna watu leo wao kazi yao ni
kuzunguka zunguka kueneza umbeya, ukiwa mtu wa malengo hautofwatilia maisha ya
mtu, maana kila dakika unalo la kufanya.
.
Ukiwa mtu wa malengo utaongeza uzalishaji, maana unajua
ulikotoka, ulipo na unapokwenda, kwanini wengi kiwango chao chakuzalisha huwa
hakiongezeki ni kwasababu si watu wa malengo.Unafanya biashara ila hauongezeki,
mtu asiye na malengo ni sawa sawa na kisiwa chenye dhahabu ila bado
hakijavumbuliwa, malengo yanakufanya upande viwango siku baada ya siku.
Watu wanaoishi kwakiasi ni watu wamalengo, mtu wa malengo
sikuzote ni mtu wa kujizuia, ukiwa mtu wa malengo utachagua, mahali pakuongea,
utachagua watu wakushinda nao, utafanya kila kitu mahali pake
1Wakorintho 9:25A
Na kila ashindaye katika michezo hujizuia katika yote.
Ili ushinde katika maisha ni lazma ujifunze kujizuia, ili
uishi maisha ya ushindi ni lazima ujifunze kuwa na kiasi, na hauwezi ukawa na
kiasi kama huna malengo, malengo pekee yanakudabisha ili uishi maisha ya
ushindi
2Timotheo 1:7
Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu naya upendo nay a moyo
wa kiasi.
Mungu ameachilia moyo wa kiasi,
moyo wakiasi unakaa kwa mtu mwenye malengo, mtu ambaye anajua anakokwenda, ukijua
unakokwenda kunavitu hutovifanya, kuna marafiki hutoongea nao, kuna chakula
hutokula, kuna maeneo hutoingia maana ni mtu wa malengo, kila kitu
unachokifanya hufanyi kwa bahati mbaya.
Zaburi 1:1
Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la
wasio haki,
Wala hakusimama katika njia yawakosaji,
Wala hakuketi kaika njia ya wakosaji
Ili ukutane na watu sahihi, malengo
yanachagua watu muhimu, ambao watafanya lengo lako litimie, mfano mwanafunzi,
lengo lake ni kusoma ni lazima akutane na mwalimu, ukiwa mtu wa malengo
hautoongea na kila mtu, ila wapo watu maalumu ambao utakutana nao.
Daudi anasema heri mtu asiye kwenda katika
shauri la wasio , kumbe hao wasio haki ni watu na ukikosa kuwa mtu wa malengo,
utakwenda katika shauri la wasio haki.
Kuna watu leo utawakuta wanashinda toka
asubuhi hadi usiku kucheza bao tu, halafu huishia kusema jamani maisha ni
magumu sana, kumbe maisha yamekuwa magumu kwasababu ya kukaa mahali penye
mizaha. Mungu anataka ubadilike ukianza kuwa mtu wa malengo utabadilika kabisa
na kuwa mtu mwingine.
Malengo ni mwongozo wa kazi yako, mtu asiyekuwa na malengo
ni sawa sawa na ndege isiyokuwa na rubani, ni sawa sawa na gari lisilokuwa na
dereva litadondoka tu, umefika mahali kila unachokifanya kinaanguka nikwasababu
umekosa malengo, malengo yanakupa uwelekeo uelekee wapi katika safari yako,
Stamina ni kiu, hamu, au huruka, mtu asiyekuwa na malengo ni
sawa sawa na gari iliyokosa mafuta, itaenda kwakusukumwa, unafanya kazi zako
lakini ndani hujisikii, kutamani kuendelea ni kwasababu huna stamina, yaani umekosa
malengo, mtu asiye na malengo siku zote anafanya vitu kivivu, anakwenda kwa
kusukumwa. Ikiwa mwanafunzi ameweka lengo la kupata division 1,
kitakachomsukuma ni hilo lengo lakupata division 1, au mwingine hana lengo
lolote, atakuwa analala hata muda wakusoma.Malengo ndiyo upako wako wa
kiutendaji.
Ukiwa na malengo utaweka akiba, mtu aliyekosa malengo
anatumia kupita kiasi, wafanya biashara wengi wanajinyima ili mitaji yao ikue,
wanaweka akiba ili siku biashara zikigoma watwae katika akiba zao. Katika
maisha kuna nyakati mbili kuna nyakati za kupata na kunanyakati za kukosa, ili
usiwe masikini, ombaomba katika nyakati za kukosa inategemeana uliweka akiba
siku za kupata, akiba si sawa sawa mvua ambayo haitumiki inasubiri kipindi
ambacho watu wanapanda ili inyeshe, akiba ni ndugu yako siku ya taabu, ukiwa
mgonjwa atakutibu, ukifiwa atakuja kukuona, ukitukanwa atakufariji.
Mungu anataka ufike mahali unakuwa mtu wa malengo.
Mungu anataka ufike mahali unakuwa mtu wa malengo.
MTU WA MALENGO
Reviewed by adam
on
Februari 01, 2017
Rating:
![MTU WA MALENGO](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiy06d2HeMJwSvaN9WdLHg8IvOpm7aqdllbheKT9jaCfGDmd7xz1lL_ck0AcEi1xxoB-PQhoIsLSUOQSm6KL4USAXVKixMpAXEt6Og36NaSbYHEUkIadDMHsaxikEwEJrcy2tkaS0wCumSq/s72-c/MSHALE.jpg)
Hakuna maoni: