Watu wengi wanajiuliuliza nguvu ya Mungu
ni nini na inawezeje kutenda kazi? Ni kwamba nguvu ya Mungu ni uwezo wa
Mungu ambao unaachiliwa kwa Neno la Mungu na kuleta matokeo kama
lilivyoagizwa na Mungu mwenyewe,matokeo ya Neno la Mungu ndiyo nguvu ya
Mungu,kwasababu neno likitumwa linaleta mabadiliko kwenye maisha ya
watu,na wengine pia wanajiuliza kwamba kuna kuguswa na nguvu ya Mungu
hivi huko kuguswa kuna maana gani ?
MAANA YA KUGUSWA
Kugusa ni ishara ya kuonyesha ili mtu
akuonyeshe kitu anagusa ili kukudhibitishia,kukupa uhakika wa kile
ambacho anakwambia,hivyo Mungu anatabia hii ya kugusa watu wake ili
awadhibitishie kwamba yeye ndiye Mungu mafano inasema.
Yeremia 33:3
“niite nami nitakuitikia na kukuonyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua” (anaposema kuonyesha ndiyo ishara ya kugusa)
Kumbe hili neno unaweza kuliweka hivi:Niite nami nitakuitikia na kukugusa katika matendo makubwa magumu usiyo yajua,matendo
makubwa magumu ndiyo matokeo ya nguvu ya neno la Mungu,hayo matokeo ya
nguvu ya neno la Mungu ndiyo uponyaji,hiyo ndiyo mipenyo ambayo Mungu
anaachilia kwenye maisha ya watu wake,unaweza ukawa na tatizo unahitaji
kuguswa tu na nguvu ya Mungu maana yenyewa ikikugusa tu mabadikliko
yanatokea kwenye maisha yako tuone mifano michache kwenye maandiko ya
watu walioguswa na nguvu ya Mungu.
1) Vipofu wawili waliomfuata Yesu alipokuwa akipita.
Mathayo 9:27-30
“Yesu alipokuwa akipita kutoka
huko,vipofu wawili wakafuata wakipaza sauti,wakisema urehemu mwana wa
Daudi.Naye alipofika nyumbani wale vipofu walimwendea Yesu akawaambia
mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia Naam Bwana,ndipo
alipogusa macho yao akawaambia kwa kadili ya imani yenu mpate,macho yao
yakafunguka”.
Kipofu
ni mtu asiyeona mbele yake anaona giza,hawa vipofu wawili
wanafananishwa na watu wasiokuwa na maono ambao hawana uhakika na maisha
yao,hawajui walikotoka kupoje wala wanako elekea kuna hali gani? Hivyo
wanaishi maisha ya kupapasa,Yesu aligusa macho yao maana yake aligusa
maono yao.Nguvu ya Mungu inapojidhihirisha mahali inashughulikia
maono.Mwingine yupo kwenye ndoa kwa Muda mrefu hajapata mtoto ukiangalia
mbele yake anaona giza kwamba hawezi kupata mtoto,Yesu akikugusa
unapata maono ya kupata mtoto,kwasababu ili shetani akupate anakuharibia
maono yako na ndiyo maana vijana wengi wanaangamia kwa kukosa
maono,wana macho lakini hawaoni maana maono ndiyo macho yanayobadilisha
maisha ya mtu.Kumbuka nguvu ya Mungu ikimgusa mtu inashughulikia maono
ya mtu,chochote unachokitaka kwa Mungu ni lazima ukione kwanza ndipo
ukipate,ukiona maisha mazuri yatakuja maisha mazuri,ukiona kupona
utapona,Yesu aligusa macho yakafunguka,nguvu ya Mungu ikikugusa utaona
kule unakoelekea.
2) Mama mkwe wa Petro amelala hawezi homa imemkamata.
Mathayo 8:14-15
“Hata Yesu alipofika nyumbani kwa
Petro,akamwona mkwe wa Petro,mamaye mkewa maelala kitandani hawezi
homa.Akamgusa mkono homa ikamwacha,naye akaondoka akawatumiakia”
Umejiuliza
kwanini ?Yesu aligusa mkono homa na ikamwacha,kwanini? nguvu ya Mungu
iligusa mkono wa Mama mkwe wa Petro homa ikamwacha,kumbe kuna kitu Yesu
alikuwa anakishughulikia kwenye mikono ya mama mkwe wa Petro,mikono
inahusika na utendaji wa kazi(kila kazi ianafanywa na mikono).Angalia
sana kuna watu wengine mikono yao imebeba laana kila wanachokifanya
hawafanikiwi mpaka wanapata homa,magonjwa kutokana na mkandamizo wa
mawazo wakutokufikia malengo yao kama mama mkwe wa Petro,kumbuka kwamba
biashara zako ni kazi ya mikono,masomo yako ni kazi za mikono,kilimo
chako ni kazi za mikono na maandiko yanasema Mungu atabariki kazi za
mikono,Yesu alipokuwa anagusa mikono ya mama mkwe wa Petro alikuwa
anashughulikia laana iliyokuwepo kwenye mikono ya mama mkwe wa
Petro.Mwambie Yesu kama alivyogusa mikono ya Mama mkwe wa Petro mwili
wake ukawa salama vivyo hivyo akuguse na wewe kazi zako zikawe salama.
MAMBO MUHIMU YA KUFANYA ILI UGUSWE NA NGUVU YA MUNGU
1)Viguse vilivyo mgusa Yesu.
Marko 5:25-34
“Na mwanamke mmoja mwenyekutokwa damu
kwa muda wa miaka kumi na miwili,na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu
wengi,amegharimia vitu vyote alivyonavyo, kusimfae hata kidogo bali
hali yake ilizidi kuwa mbaya bali aliposikia habari za Yesu,alipitaa
katika mkutano kwa nyuma akaligusa vazi lake,maana alisema nikiyagusa
mavazi yake tu nitapona,mara chemchemi ya damu yake ikakauka,mara
akafahamu nafsini mwake kwamba amepona msiba ule,na mara Yesu hali
akifahamu nafsini mwake ya kwamba nguvu zimemtoka,akageuka kati ya
mkutano,akasema ni nani aliyenigusa? wanafunzi wake wakamwambia Je
wawaona mkutano wanavyo kusongasonga,nawe wasema ni nani aliye
nigusa.akatazama pande zote ili amwone yeye aliyetenda neno hilo.Yule
mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka,akijua lililompata,akaja
akamwangukia,akamweleza kweli yote,Akamwambia binti imani yako
imekuponya,enenda zako kwa amani uwe mzima,usiwe na msiba wako tena."
Kuna
nguvu katika kuvigusa vilivyomgusa,ili nguvu ya Mungu ikuguse kanuni
mojawapo ya kiroho ni kugusa vilivyomgusa,mwanamke mwenye kutokwa damu
aligundua hii kanuni ya kiroho akagusa upindo wa mavazi yake Yesu,nguvu
zikamtoka Yesu kupitia kwenye mavazi zikamgusa mwanamke.Huyu mwanamke
alitengwa na jamii yake kwasababu ya kutokwa damu na alilipa gharama ya
damu kumwagika,kwa kuzunguka mahospitalini na kukutana na waganga wa
kila namna lakini ugonjwa wake haukupona,ila alipopata habari za Yesu
alisema nikiyagusa mavazi yake tu nitapona,angalia vizuri mavazi
yalikuwa yamemgusa Yesu kile kitendo cha kugusa kilicho mgusa nguvu ya
Mungu ikamfungua mwanamke,kumbuka mwanamke hakugusa ngozi bali vazi la
Yesu.Vazi la Yesu limepewa nafasi ya kugusa ngozi ya Yesu ndilo limebeba
nguvu inayobadilisha,na unapogusa vazi la Yesu automatically nguvu
zinamtoka Yesu na kukugusa,unaweza ukawa unasema mbona naingia kanisani
ila ugonjwa wangu hauponi swali ni kwamba umevigusa vilivyomgusa? Na
ndiyo maana wengine wakiomba kidogo Mungu anasikia maombi yao na
kuyajibu kwasababu wamevigusa vilivyomgusa hata ndani ya kanisa
tutaendelea kutofautiana katika wengine watafanikiwa sana na wengine
watafanikiwa kidogo kwasababu ya kutofautiana katika kuvigusa vilivyo
mgusa,wataingia wagonjwa watatoka wagonjwa na wengine wazima.Hata siku
ile mwanamke hakuwa mgonjwa peke yake,walikuwepo wengi lakini aliyegusa
vilivyomgusa ndiye aliyefunguliwa.
Luka 6:16
“Na makutano wote walikuwa wakitaka kumgusa,kwasababu uweza ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote."
Je unataka uweza wa Mungu ukifikie? mguse
ili ukufikie hawa walikuwa wakimgusa na uweza wa Mungu ulikuwa ukimtoka
na kuponya magonjwa yao.Watu wengi wanapenda kuombewa lakini hawapendi
kulipa gharama ya kugusa vilivyomgusa,hata kama mtumishi wa Mungu
anakuombea hakikisha una vigusa kwanza vilivyomgusa Mungu ili maombi
yalete matokeo,haijarishi ni tatizo gani wewe gusa tu vilivyomgusa ipo
nguvu inayobadilisha katika vile vilivyomgusa Yesu.Mtu anaweza akawa
anajiuliza hivyo vitu vilivyomgusa Yesu ni vitu gani? Au hayo mavazi
aliyoyagusa mwanamke yalikuwa yanamaanisha nini?,tuangalie kwa undani
maana Roho mtakatifu anataka akufundishe kitu.
Kuguswa na Nguvu ya Mungu(Sehemu ya kwanza)
Reviewed by adam
on
Januari 17, 2017
Rating:
Hakuna maoni: