NEWS

Mtu wa Rohoni

                                                        MTU WA ROHONI

Mtu wa rohoni uzazi wake hautokani na namna na taratibu za Dunia bali uzazi wake unatokana na Roho wa uzima, ndiyo maana vitu vingi yeye anavyovifanya yupo tofauti kabisa na dunia, tambua kwamba endapo watu tunaishi mwilini, ila tunafanya mambo si kwakuufuata mwili, bali Roho wa uzima, pale unapomfuata Roho wa uzima maana yake wewe ni mtu Rohoni, huendi kwa kuufuata mwili.
MAMBO MATATU AMBAYO MTU WA ROHONI ANAKUA KINYUME NAYO.
                                                         Yohana 1:12-13.
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyia watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake.Waliozaliwa si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu bali ya Mungu.
                                 1.Uzazi wa kibailojia { Biological birth}




Maandiko yanasema waliozaliwa si kwa damu. Tunajua baiolojia inasema mtu ili azaliwe anahitaji mume na mke wakutane, maana yake zikutane damu za jinsia mbili tofauti mtu anazaliwa kwa jinsi hiyo, lakini mtu wa Rohoni hazaliwi kwa namna ya bailojia ndiyo maana anaweza akafanya mambo makubwa hadi baiolojia ikashangaa
Mfano.
Bailojia haiamini kwamba mtu anaweza akakaa na njaa siku arobaini, Bali tunamwona Musa mtu wa Rohoni( aliye zaliwa katika roho) anafunga siku arobaini bila kula wala kunywa. Tunamwona Eliya mtishibi anafunga siku nyingi,
Tunamwona  Bwana wetu Yesu Anafunga siku arobaini bila kula wala kunywa.

         Luka 4:1-2.
Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani akaongozwa na Roho Mtakatifu hadi jangwani, mahali ambako kwa siku arobaini alikuwa akijaribiwa na Ibilisi. Kwa siku zote hizo hakula cho chote, hivyo baada ya muda huo akaona njaa.
Tunamwona Danieli mtu katika Roho anafunga siku ishirini na moja.
Danieli 10:1-3
Wakati huo, mimi Danieli, nikaomboleza kwa majuma matatu. Sikula chakula kizuri, nyama wala divai havikugusa midomo yangu, nami sikujipaka mafuta kamwe mpaka majuma matatu yalipotimia.



Vinavyoshindikana kwa baiolojia kwa mtu katika Roho vinawezekana..
Bailojia haiamini kwamba mtu akifa anaweza akafufuliwa, Tunamwona Yesu mtu wa Rohoni anamfufua Lazaro aliyekufa na kuzikwa kwa muda wa siku nne.
Yohana 11:43-44
Baada ya kusema haya, Yesu akapaaza sauti Yake akaita, ‘‘Lazaro, njoo huku!’’ Yule aliyekuwaamekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake. Yesu akawaambia, “Mfungueni, mwacheni aende zake.’’


 Elisha mtu wa rohoni anamfufua mtoto wa mwanamke mshunem.
2 wafalme 4:33-35.
Akaingia ndani, akajifungia yeye na yule mtoto, akamwomba BWANA. Kisha akapanda kitandani akalala juu ya yule mtoto, mdomo wake juu ya mdomo wa mtoto, macho yake juu ya macho ya mtoto, mikono yake juu ya mikono ya mtoto. Naye alipojinyosha juu yake, mwili wa mtoto ukapata joto. Elisha akajiondoa juu yake na kuanza kutembeatembea ndani ya chumba na kisha akarudi tena kitandani na kujinyosha tena juu ya mtoto mara nyingine. Mtoto akapiga chafya mara saba na akafungua macho yake.

 Eliya mtu wa Rohoni anamfufua mtoto wa Mwanamke mjane wa Sarepta.
1 Wafalme 18:19-23
Eliya akamjibu, “Nipe mwanao.’’ Eliya akampokea kutoka kifuani mwake, akambeba mpaka chumba cha juu alipokuwa anaishi, akamlaza kitandani mwake. Kisha akamlilia BWANA,akasema “Ee BWANA wangu, je, pia umeleta msiba juu yamjane huyu ninayeishi pamoja naye, kwa kusababisha mwanaye kufa?” Kisha akajinyoosha juu yakijana mara tatu na kumlilia BWANA, akisema, “Ee BWANA wangu, nakuomba roho ya huyu kijana imrudie!’’ BWANA akasikia kilio cha Eliya, na roho ya kijana ikamrudia, naye akafufuka. Eliya akamtwaa kijana na kumbeba kutoka chumbani mwake akamshusha kumpeleka kwenye nyumba. Akampa mama yake na kusema, ‘‘Tazama, mwanao yu hai!’’

Baiolojia imeshindwa kutibu ukimwi lakini mtu wa Rohoni anatibu ukimwi.
Luka 1:37.
Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana.

Mathayo 16:13-17.
Basi Yesu alipofika katika eneo la Kaisaria Filipi, akawauliza wanafunzi wake, “Watu husema Mwana wa Adamu ni nani?” Wakamjibu, “Baadhi ya watu husema ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya na bado wengine husema, ni Yeremia au mmojawapo wa manabii.’’ Akawauliza, ‘‘Je, ninyi, mnasema mimi ni nani?’’ Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.’’ Naye Yesu akamwambia, ‘‘Heri wewe, Simoni mwana wa Yona, kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali na Baba yangu aliye mbinguni. 

Tunamwona Yesu anauliza wanafunzi wake kwamba wanamwita yeye ni nani? Kila mmoja akataja namna ambavyo Yesu wanamwita mitaani, Pia yeye akawauliza ninyi mnaniita mimi nani? Petro akajibu wewe ndiwe kristo mwana wa Mungu aliye hai.
Yesu anamwambia umebarikiwa Petro kwa kuwa mwili na damu { anaposema damu anazungumza baiolojia} Havikukukufunulia hili bali Baba yangu aliyembinguni anaposema Bali anamaanisha andiko hili.
1 wakorintho 2:14.
Mwanadamu wa tabia ya asili { tabia ya kibaiolojia} hayapokei mambo ya Roho, maana kwake huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya mwili.

Petro aliyatambua kwa kuwa alikuwa ni mtu wa rohoni,

                                             VITA YA KIBAIOLOJIA {BIOLOGICAL WAR}.


Hapo zamani vita ilikuwa inapigwa kupitia siraha kama vile mapanga, mikuki, marungu, mishale mabomu na Bunduki, Hivi vitu ndivyo vilikuwa vikiwaendesha wakristo na kuwakosesha raha watu waliyozaliwa katika roho.
Tunamwonashetani anavyotetemesha taifa la Israel kwa kumwinua Goriath ambaye alitumia panga, chapeo.
Lakini sasa shetani ameendelea baada ya kutumia hivyo, sasa yeye anatumia vita ya kibailojia ili kuwakamata watoto wa Mungu. Kwa kutengeneza magonjwa ya kila namna, shetani sasa anashinda maabara ili agundue magonjwa ya kuwasumbua watu wa Mungu, kila siku magonjwa mapya yanaibuka ambayo yanatesa watu hata watu waliyozaliwa katika Roho.
Mfano Ayubu.
Ayubu 2:7
Basi Shetani akatoka mbele za BWANA
naye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya
tangu nyayo za miguu yake hadi utosi
wa kichwa.

Hii ni vita ya kibaiolojia, shetani anampiga mtu wa rohoni ambaye ni Ayubu kwa majipu, shetani amekuwa mtesaji sana wa watoto wa Mungu, kila magonjwa anagundua ili apate kuwaangusha watu Mungu, anatumia vita ya kibailojia ili awanase wengi.
 
Mawasiliano kwa huduma zaidi
piga 0764901546 au email: adstep4@gmail.com au adstep100@gmail.com

MAFUNDISHO HAYA YATAENDELEA




Mtu wa Rohoni Mtu wa Rohoni Reviewed by adam on Februari 09, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.