NEWS

Aina nane za maombi kwaajili ya kondoo



Yesu ndiye mfano wa kuigwa, unapokuwa na kundi na unaposimama nalo katika maombi, wachungaji wengi hawajui namna ya kuombea kondoo au niseme watu wengi ambao Mungu amewakabithi watu hawajui namna yakuombea kondoo.Na wengi wao hawaombei kondoo wala hawajali kondoo.


Yohana 10:12-13
Mtu wa mshahara,wala si mchungaji ambaye kondoo si mali yake, amwonapo mbwa mwitu anakuja, hukimbia na kuwaacha kondoo na mbwa mwitu huwakamata  na kulitawanya. 

 
Ukiwa mchungaji wa mshahara ni rahisi sana kuliacha kundi, wakati mbwa mwitu wajapo, lakini mchungaji ambaye kondoo ni mali yake anasimama na kondoo hata kuutoa uhai wake,
Mbwa mwitu ni watu wabaya ambao shetani anawatumia kutawanya kondoo, mbwa mwitu wanaweza wakaingia hata ndani ya kanisa, mbwa mwitu kazi yake wao ni kutawanya, siku zote.







1 Samweli 17:34-35
Lakini Daudi akamwambia Sauli,
Mtumishi wako amekuwa akichunga kondoo za
baba yake. Wakati simba au dubu alipokuja na
kuchukua kondoo kutoka katika kundi,
nilifuatia, nikampiga na nikampokonya kondoo
kwenye kinywa chake. Aliponigeukia,
nilimkamata nywele zake, nikampiga na
kumwua

 
Mchungaji ni lazima ujue kushughulikia wanyama wakali wakutawanya kundi, wanaokula kondoo za kundi. Daudi alikuwa ni mchungaji aliyekabithiwa kondoo na Baba yake ili awatunze na kuwalisha, Mungu ambaye ni Baba yetu amekukabithi kundi ili ulitunze na kulilisha lakini wewe haushughuliki na wanyama wakali bali unawaacha wafanye jinsi wanavyoweza  kufanya juu ya kondoo. Daudi alinyanganya kondoo kwenye kinywa cha simba, ilifika hatua kondoo ameshaakamatwa hakumwacha kondoo aliwe alipambana na simba hadi akamuua, Mungu anataka uuwe simba na dubu wanaonyemelea kondoo, usikubali kondoo akaliwa na simba na dubu.
Mungu alikuwa pamoja na Daudi, Ndivyo ambavyo yeye yupo pamoja na wewe leo, kila unapopigania  kondoo.

Mathayo 28:20
Tazama Mimi niko pamoja
nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa daharii.


SEHEMU ZA KUGUSIA JUU YA KONDOO KATIKA MAOMBI.
1.Kondoo wamjue Mungu wa kweli na Yesu Kristo.

Yohana 17:3.
Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue Wewe uliye Mungu wa
 pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.

 
Kondoo nyingi za kundi zimejaa kutokumjua Mungu, Yesu katika maombi yake aliliona hili akaombea kundi limjue Mungu wa kweli, na Yesu Kristo, Wengi wanaabudu wasichokijua wanadhani ni Mungu wa kweli waliyemshikilia kumbe si wa kweli.
Yapo mafundisho potofu ambayo yanapotosha kondoo za Mungu, kama ikiwa kondoo hawajamjua Mungu ni rahisi hao kondoo kutoka nje ya zizi, Kondoo aliyemjua Mungu shatani hawezi akamtoa nje ya zizi.

Yohana 10:4,27
Akiisha kuwatoa wote nje,
hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa
kuwa wanaijua sauti yake
Kondoo Wangu huisikia sauti
Yangu nami nawajua, nao hunifuata

 
Yesu anasema kondoo wake wanaijua sauti yake, unakondoo wengi ila mpaka sasa hawaijui sauti ya Yesu, ila wanazijua sauti za wageni, ni kazi kwako kuomba ili kondoo waijue sauti ya Yesu, zipo sauti nyingi leo duniani ambazo kondoo tulionao wanazisikiliza hawazikimbii ni kwasababu hawajajua kutofautisha kati ya sauti ya Yesu na sauti za wevi.
Hili ni ombi la muhimu sana kila unapokaa kwenye maombi, ukiombea kundi la Bwana.
2.Kondoo walindwe  na nguvu ya Mungu.

Yohana 17:11.
Kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa.

 
Yesu anaomba ulinzi kwa kondoo, anasema mimi sipo tena ulimwenguni, maana yake kimwili sitokuwa nao, kimwili Yesu ambaye ndiye mchungaji wetu hayupo pamoja na sisi ila kiroho anaruhusu nguvu za Mungu zitufunike.
Ukweli upo mbali na kondoo kimwili, wewe unakaa mahali pengine, na kondoo zinakaa mahali pengine, lakini kwa maombi unauwezo wakuwafikia wote na ukawalinda, ukisha omba ulinzi kwa Mungu haitakiwi uwe na wasiwasi tena juu ya kondoo maana nguvu ya Mungu ndiyo inayotunza
Kwanini wachungaji wengi wanawasiwasi juu ya kondoo ni kwasababu hawombei kondoo, hawalindi kondoo,Yesu alipotuombea kwa Mungu hakuwa tena na wasiwasi.
3.Umoja wa kondoo.

Yohana 17:11,21,23
Kondoo Wangu huisikia sauti
11.Yangu nami nawajua, nao hunifuata.
21.ili wawe na umoja kama
vile Wewe Baba ulivyo ndani Yangu na
Mimi nilivyo ndani Yako, wao nao wawe
ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya
kuwa Wewe ndiye uliyenituma Mimi
23Mimi ndani Yako na Wewe ndani Yangu,
ili wawe wamekamilika katika umoja na
ulimwengu upate kujua ya kuwa
umenituma, nami nimewapenda wao kama
unavyonipenda Mimi

 
Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, Yesu anaomba umoja wa kondoo, ikiwa Mungu hajawapa kondoo umoja, hawawezi wakashikamana ndiyo maana leo katika makanisa tunawashirika waliotengana, wasiozikilizana, wanaogombana kwasababu umoja umekosekana Yesu anasisitiza swala la umoja, anasema achilia umoja kwakondoo,
Yesu anazungumza faida za Umoja, anasema kwa umoja watu watasadiki kwamba Yesu alikuja kwa ulimwengu, kwa umoja kondoo wanakamilishwa, kwa umoja kondoo wanakuwa kama Baba na Yesu.
Ni nguvu ya Mungu pekee inayoweza ikaleta umoja katika kondoo, na maombi pekee ndiyo yanayoalika msaada wa Kimungu ili kondoo zishikane, ukiomba umoja kondoo watapendana bila kujali tofauti zao lakini umoja ukikosekana kondoo watakimbia katika zizi.
Tunamakanisa leo yasiyojaa kondoo, yamekaa miaka mingi, na mengine yanajaa kwa kipindi fulani halafu baada ya Muda mfupi watu wote wanatawanyika, chanzo mara nyingi ni kwasababu ya kukosa umoja ndani ya kanisa hivyo shetani anatumia hiyo kusambalatisha kanisa.

4.Furaha ya Yesu itimizwe ndani ya kondoo.

Yohana 17:13.
Ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.

 
Yesu aliliona hili, kwamba kondoo akikosa furaha ni rahisi kurudi nyuma, ni rahisi kutoka nje ya zizi, kama furaha ya Yesu ikitimizwa ndani ya kondoo, kondoo hawatatamani kutoka nje ya zizi, furaha ya Yesu ni kitu gani basi? furaha ya Yesu nikuona kondoo wanafanikiwa kimaisha, kondoo wengi furaha imeondoka kwasababu ya maisha kuwa mabaya, maisha yanapokuwa mazuri kondoo wanafurahia, hapo Yesu anajisikia furaha unapoomba furaha ya Yesu itimizwe ndani yao, unamfanya Mungu awape maisha bora siyo bora maisha, hili ni ombi la muhimu unapombea kondoo.

5.Watakaswe na kweli ya Neno la Mungu.

Yohana 17:17
Uwatakase kwa ile kweli, Neno Lako ndilo kweli.

Mungu anataka kondoo iliyotakasika, siyo kondoo iliyochafuka, ni kazi ya mchungaji kuwatakasa kondoo kwa njia ya maombi, unapoomba ombi hili unaalika mbingu zishughulike na kondoo mmoja mmoja aliyemchafu ndani ya kanisa.
Yesu anamwambia Mungu uwatakase na kweli yako, Kuna muda Mungu anatamani angesikia ombi hili kutoka kwako, ni kweli wewe ni mchungaji je unauhakika hao kondoo ulionao wametakasika? au je hujui kitu? Unapokaa kwenye maombi Mungu anafungua mlango wa kondoo kutakasika, kanisa lako linasifika kwakukalisha wazinzi, kanisa lako linasifuka kwakukalisha walev, linasifika kwakukalisha wachawi, linasifik kwakukalisha waongo, watu wasiotakasika, wenyesifa mbaya mitaani, lakini Yesu alifahamu hili hakutaka kanisa la mtindo huo akaomba watakaswe na kweli, unapokaa kuomba Mungu mwenyewe ndiye anayetakasa kwa njia ya maombi yako.

6.Mungu awatukuze kondoo.

Yohana 17:22
Utukufu ule ulionipa nimewapa wao.

Utukufu ule aliopewa Yesu ameachilia kwakondoo, hili ni ombi la muhimu sana Mungu awatukuze kondoo kama alivyomtukuza Yesu, awainue kondoo kama alivyomwinua Yesu, Yesu anataka kondoo wafike kwenye kiwango chake. Kama Yesu alivyo ndivyo kondoo wawe, kama Yesu anavyofahamika ndivyo na kondoo wafahamike.Kondoo isipotukuzwa na Mungu ni rahisi kutoka nje ya zizi
Niombi ambalo mchumgaji au kiongozi yeyote wa kundi anatakiwa alichukulie uzito.

7.Mungu aongeze upendo kwa kondoo.

Yohana 17:23.
Ukawapende wao kama ulivyonipenda mimi.

Yesu anataka upendo wa Mungu usipungue kwa kondoo, kama Mungu atapunguza upendo wake kwa kondoo yeyote kanisani, hiyo kondoo itatoka nje ya zizi, iwapo katika kondoo kama Mungu ataona dhambi kwa kondoo yeyote ndani ya kanisa, Mungu akazidishe upendo wake zaidi, maana upendo wa Mungu unaongeza neema ya kushinda, kilichomfanya Mungu amtume mkombozi ulikuwa ni upendo, upendo ukizidi kwa kondoo Mungu atamkomboa kondoo aliyefungwa na vifungo vya dhambi na mapepo. Omba ombi hili mara kwa mara ipo nguvu ambayo itamwinua hata huyo mnyonge ndani yakanisa baada tu ya upendo wa Mungu kuongezeka.
8.Wawe pamoja na Yesu popote alipo.

Yohana 17:24
Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo.

 
Yesu anasema popote alipo awe pamoja na kondoo, Yesu yupo mahali penye usalama, ukomba ombi hili utawafanya kondoo wako wawe mahali penye usalama, kondoo nyingi leo hazipo salama kwasababu zipo mbali na Yesu, kazi ya Yesu ilikuwa kuomba, kazi yako ni kuomba Mungu anawakusanya kondoo ulio nao na kuwaweka karibu na Yesu.
Ninayofuraha sana ikiwa umesoma na kutendea kazi hizi aina saba za maombi unayotakiwa kuomba kwaajili yakondoo, ni kazi kwako kuombea ili Mungu alete mabadiliko katika kundi ulilokabithiwa na Mungu ikiwa utafanya haya maombi kwa mfululizo bila kukoma utaona ambavyo Mungu ataleta mabadiliko kwa kondoo ulizonazo, hata yule uliyedhani anakichwa kigumu Mungu atamfungua.



Aina nane za maombi kwaajili ya kondoo Aina nane za maombi kwaajili ya kondoo Reviewed by adam on Januari 17, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.