Kunena kwa lugha ni lugha ya rohoni ambayo Roho mtakatifu anaitumia kutuombea kwa Mungu, kwa hiyo basi kama ni lugha ya rohoni, mtu wa mwilini hawezi akaisikia, wala akatambua isipokuwa na yeye yupo rohoni.Kunena kwa lugha ni maombi ya siri ya mtu,ukiomba kwa lugha yako kila mtu atasikia, maana ni lugha yako ya asili inayofanana na watu wengine.
Watu wengi leo wananena kwa lugha, lakini hawajui kutofautisha, swala la kunena kwa lugha, na wengine wapowaona watu wananena kwa lugha wanasema ni lugha yamashetani, hapana kunena kwa lugha si lugha ya mashetani bali kwa mtu aliyeokoka ni kipawa cha Mungu kwa Roho wake mtakatifu.
Kuna aina mbili za kunena kwa lugha.
1.Kunena kwa lugha kama ishara.
Marko 16:17
Naishara hizi zitafuatana na hao waaminio kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya.
Yesu anazungumzia kunena kwa lugha mpya kama ishara, ishara ya kwamba ninyi mumemwamini Yesu kama mwana wa Mungu ni kunena kwa lugha, kunena kwa lugha ni kitambulisho cha mtu aliyemwamini Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake, ishara ya kunena kwa lugha nikwaajili ya watu wasiomwamini Yesu.
Wakorintho 14:22.
Basi hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio bali kwao wasio amini
Kunena kwa lugha kama ishara kupo si kwaajili yawaaminio, bali kwaajili ya wale wasio amini ili wapate kuamini, Wengi ndani ya kanisa hunena kwa lugha kama ishara.
2.Kunena kwa lugha kama karama.
Kunena kwa pili kwa lugha ni kunena kama karama, kunena kwa lugha kama karama Mungu anamtumia mtu ili kufikisha ujumbe kwa mtu fulani, au kanisa, kunena kwa lugha kama karama ni huduma ya Roho mtakatifu ndani ya mtu kuweka wazi mambo yaliyokuwa gizani.
1wakorintho 12:4-5 na 10d
Basi panatofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena panatofauti za huduma nai Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti zakutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
10d
Mwingine aina za lugha.
Hivyo kupo kunena kama ishara na kunena kama karama, kunena kama karama Roho mtakatifu anatenda kazi,
Mfano siku ile ya pentekosti, mitume na wale wanafunzi wengine walinena kwa lugha kama karama, ile haikuwa ishara, maana watu walisikia lugha zao, pale Roho mtakatifu alikuwa anatenda kazi, ya kuwafikia mataifa kwanjia ya aina za lugha.
Watu walikiri ya kwamba mbona hawa wanaongea lugha zetu watu ambao kwa asili si wamakabila yetu, Kunena kwa lugha kama karama Roho mtakatifu anatenda kazi.
Mfano kuna mwanamke mmoja alipokea taarifa yakamba kijana wake nchini marekani anaumwa, yupo maututi na muda wowote ajiandae kupokea maiti.
Kwa huyo mwanamke zilkuwa ni habari za kusikitisha sana kwake, siku hiyo huyo mwanamke alienda ibadani, maana ilikuwa ni siku ya jumapili, ulipofika muda wa neno la Mungu mchungaji akasimama madhabahuni, mchungaji alianza kuomba mara mchungajia akaomba kwakunena kwa lugha, kwa muda kama wa dakika kumi hivi, baadaye mchungaji akanyamaza.
Mchungaji alipotaka kuendelea na kufundisha neno, yule mama akanyosha mkono akilia na kutetemeka, akasema natakaka nishuhudie jambo ambalo Mungu amanitendea, akasimama na kusema pindi mchungaji aliposimama na kuomba alipoanza tu kunena kwa lugha alikuwa anaongea kabila letu, ambayo tafsiri yake ni hii wewe mwanamke ambaye umeambiwa ujiandae kupokea maiti maana mtoto wako yuko maututi nchini marekani, sasa kwanzia muda huu mtoto wako ni mzima ugonjwa alio nao amepona.
Watu siku hiyo walishangaa sana kwamba hayo mambo yanawezakanaje.
Kunena kwa lugha kama karama ni Roho anafikisha ujumbe, unaweza ukaenda mahali ambapo, lugha yako yakukulia haipo na Roho anataka awafundishe watu neno, awaokoe wenye dhambi Roho mtakatifu atatumia karama ya kunena kwa lugha.
Hivyo kunena kwa lugha kama karama ni kifaa cha Roho mtakatifu katika kutenda kazi yake ya injiri na udhihilisho, wanguvu za Mungu, wakati kunena kwa lugha kama karama ni ishara ya mwamini, wengi katika makanisa wananena kwa lugha kama ishara si kama karama, maana kunena kwa lugha kama karama ni lazima umtafute Mungu, maana ipo kwaajili ya shughuli maalumu.
Kwa mawasiliano na huduma:Email:adstep100@gmail.com
Simu:0764901546
AINA ZA KUNENA KWA LUGHA KATIKA MAOMBI.
Reviewed by adam
on
Februari 19, 2017
Rating:
![AINA ZA KUNENA KWA LUGHA KATIKA MAOMBI.](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5O6eTELrHs-fo1IWK4tWpm7apqcr-ATgwV3K1_YFGvIs-_Yn-mKVtBMNqlGZiakzLcLJNjp4wXmSAGaSueyObipOwaEmU-4-v5uUoHY3Hz74Ylmf50cTzVHGVxb20ZX7xbqRgGfN7zIVv/s72-c/images.jpg)
Hakuna maoni: