Ni swali la msingi sana, kwa wale wanaohudumia watu wa Mungu, kwa kuwalisha Neno la Mungu, je hadi leo unajua unaweza kulisha watu wangapi? labda idadi ya watu unao wataka kanisani kwako, ni kubwa kuliko chakula ulicho nacho, au idadi ya watu ulio nao ni ndogo na chakula ulicho nacho ni kingi, hivyo kininge kinaharibika.
Nimeona watu wengi sana wana malengo yakuwa na maelfu ya watu makanisani mwao, lakini swali hili hawajiulizi, wanafikiri watu wanakuja kwasababu ya kuwa na malengo, kumbe watu wanakuja kwasababu unaweza kuwalisha chakula wakashiba.
Na wengine wanachakula cha kutosha lakini, idadi ya watu waliyo nayo inadhohofisha chakula hicho ndani yao
Mungu anataka kama atakupa watu elfu kumi asiwepo hata mmoja atakaye sema mimi leo sijapokea, kila mmoja aseme hakika nimeshiba Mungu amenitembelea.
Wakati mmoja Yesu alikuwa na wanafunzi wake na mkutano mkubwa wa watu ulikuwa umemzunguka pande zote, na muda huo watu walikuwa na njaa sana mwanafunzi mmoja akamwambia Bwana waage watu waende kwenye vijiji wakajinunulie chakula, Yesu akamwambia wapeni ninyi chakula, wakasema hatuna chakula cha kutosha ila samaki wawili na mikate mitano, akawambia waketisheni kwenye makundi, baada ya mitume kuwaketisha kwenye mekundi akaibariki, wakala mkutano mzima na masazo yakabaki, walikula wanaume 5000 bila kuhesabu wanawake na watoto, kama kwa makadilio walikuwa ni watu zaidi ya 50000 kama wangehesabiwa wanawake na watoto. Yohana 6:1-14
Unaweza kujiuliza kwanini wewe mara nyingi watu wanakuja na kondoka kanisani kwako, lazma ujue idadi ya watu unaoweza kuwalisha, hii itakusaidia sana kuwa mtumishi mwenye hekima katika huduma.
Siku zote Yesu alikuwa anafanya huduma za injili mahali palipo jaa watu, si mahali ambapo watu ni haba, maana alijua idadi ya watu anaoweza kuwalisha, ukijua idadi ya watu unaoweza kuwalisha hutofungua kanisa mahali pasipo kuwa na watu, utafungua mahali ambapo watu wapo maana unaweza kuwalisha bila shaka.

JE! UNAWEZA KULISHA WATU WANGAPI ?
Reviewed by adam
on
Machi 27, 2017
Rating:
![JE! UNAWEZA KULISHA WATU WANGAPI ?](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEia5iYqk_8Sb7rmzeI1uKx8GdDMYhGvdJLBFVKNBGbDmmebmCzanZxt_dGhNHlo2PaJgM2izT_rlHVyxejdr0a1VQJ_6zJMiVV2KiqNbEsaW5IGeH2lDMKnqEMojN2dCbjnImj3F-ALF80u/s72-c/imagers.png)
Hakuna maoni: