Si kwamba utashinda tayari umeshashinda, si katika moja katika yote, haijarishi ni jambo gani gumu unapitia, wewe ni mshindi. umezaliwa kuwa nyota haijarishi maisha unayopitia sasa yapoje. acha kujidharau, hata kama wengine wanakudharau, acha kujushusha hata kama wengine wana kushusha.
Warumi 8:37.
Lakini katika mambo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
KUJITAMBUA.
Tatizo la wakristo wengi leo si kukosa fedha, tatizo la wakristo wengi leo si kukosa kazi, tatizo la wakristo wengi leo si kukosa uponyaji tatizo la wakristo wengi wa leo ni kukosa kujitambua, hapo ndipo shetani amewabana.
Mungu anasema katika mambo yote wewe ni mshindi, kumbe swala la kazi limesha isha, swala la ndoa leo limeshaisha, Mungu anachotaka ujitambue, kwamba wewe ni mshindi, kama ukijitambua ni rahisi kupata kazi, ni rahisi ndoa yako kuwa salama, siku ile shetani anamjaribu Yesu, alimwambia kama wewe ni mwana wa Mungu amuru jiwe hili liwe mkate.
Shetani alijua kabisa kwamba Yesu ni mwana wa Mungu, na jiwe kuwa mkate ni rahisi kwa watoto wa Mungu, ila shetani alichokuwa anajaribu ni kuona Yesu anajitambua, akajua kwamba Yesu anajitambua hivyo akakubali kushindwa.
Shetani huwa anakubali kushindwa pale tu atakapoona kwamba wewe umejitambua kwamba ni mtoto wa Mungu na ya kwamba watoto wa Mungu ni washindi.
MAMBO MATANO YANAYOONESHA KWAMBA UNAISHI MAISHA YA USHINDI.
1.Nyimbo unazoimba.
Zipo nyimbo za washindi, na zipo nyimbo za walioshindwa, huwa unapopitia changamoto ni nyimbo zipi unaimba, unaimba kama mtu aliyevushwa au kama mtu anayefia kwenye changamoto.
Waamuzi 4:24 na 5:1
Mkono wa wanawaisraeli ukazidi kupata nguvu juu ya yabini, mfalme wa kaanani, hata walipokuwa wamemwangamiza Yabini, mfalme wa kaanani.
Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu, wakaimba siku ile.
Baada ya kumshinda mfalme Yabini waliimba, nyimbo za ushindi, zipo nyimbo za washindi, Mungu anasema sisi ni washindi na zaidi ya kushinda, unapokutana na changamoto unaimba nyimbo gani.
Je ukiwa na ugonjwa ambao madaktari wamekwambia kupona haiwezekani, unaimba nyimbo ya Remi, "Kifo kifo hakina huruma", au "unapaza sauti yako ukiimba Yesu ni wangu wauzima wa milele", hata kama utasa umekuja kwako, bado wewe ni mshindi imba nyimbo za washindi, nyimbo za washindi zina yeyusha utasa, nyimbo za washindi zinazuia ajari, nyimbo za washindi ni unabii, nyimbo za washindi zinaondoa visiki njiani.
Paulo na Sila gerezani, waliimba nyimbo za sifa, nyimbo za kumtukuza Mungu. nyimbo za washindi, wapo ndani ya gereza wanaimba wema wa Yesu umenizunguka hawasemi gereza limenizunguka, wapo gerezani wanaimba Yesu wabaraka.
ITAENDELEA
WEWE NI MSHINDI
Reviewed by adam
on
Aprili 09, 2017
Rating:
![WEWE NI MSHINDI](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiASv238miT9BaV0KcdVZ40feQ0Wi0JAQSqYyvR7fJjU9htkWVjx4FutTgWXq3B_bACdueb-srCamLUzdOmPq12zDAHdXKzu8Zc0nCmUMlzOoUVwLVC5ttaO2CofWV2zb0LTSWmtfh7diZT/s72-c/imagecs.png)
Hakuna maoni: