NEWS

NEEMA ILIYOPO 2017

KUIFAHAM NAMBA SABA.
Namba ni unabii, kila kitu katika maisha kimefungwa ndani ya namba,kila namba inamaana kiunabii, kila namba inaneema yake, Mara nyingine unaweza kupitia magumu au mepesi kulingana na neema iliyopo kaika hiyo namba.
Tunaenda 2017 tutaangalia namba 7 maana namba saba ina maana kiunabii juu ya maisha ya watoto wa Mungu. Zipo baraka za Kimungu mahali popote itakaposoma namba saba ukijua neema iliyopo 2017 utatembea katika hiyo neema.
Maana jambo lolote la Kimungu ukilifanya pasipo ufahamu haliwezi kuleta matokeao, ukifahamu neema ya namba saba ni rahisi kutembea katika hiyo neema.

Namba saba ni namba ya Mungu, kama ni namba ya Mungu basi ni namba ya ukamilifu, vitu vingi alivyovifanya Mungu amevikamirisha katika namba 7, namba saba imetajwa mara 735 katika biblia,wiki ina siku saba, na siku ya saba ni ya Mungu, Neno uumbaji limetumia mara saba katika biblia.Kuna wazee saba katika biblia agano la kale waliosemwa kwamba ndiyo watumishi wa Mungu.
Katika kitabu cha waebrania Paulo ametaja vyeo saba vya Yesu.Kuna maajabu saba ya dunia, upinde wa Mvua ni rangi saba, dunia imeudwa na mabara saba, zipo bahari saba katika dunia, siku ya saba ndiyo Mungu aliyostarehe katika uumbaji wake.

MAMBO YATAKAYOTOKEA 2017 KAMA NAMBA 7 YA UNABII ILIVYO.
1.Watu watastarehe.
Kila inaposoma namba saba watu lazima wastarehe, haijarishi wewe ni mtumwa au umebeba mizigo ya namna gani, 2017 ni mwisho wa kukumbatia mizigo uliyo nayo, Mungu anaenda  kukustarehesha, mwaka 2017 ni mwaka ambao umebeba pumziko, ni kimvuli kwa wale waliochoka, ni chakula kwa wenye njaa, ni fursa kwa waliokosa kazi.

Mwanzo 2:2.
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba akaacha kazi yake yote aliyoifanya.
Iliposoma saba mbele za Mungu, Mungu alistarehe baada ya tabu za siku sita, umepitia tabu za mwaka 2016, katika hiyo miaka sita toka 2010 Mungu anakustarehesha 2017, wewe uliye tasa Mungu anakustarehesha na mateso ya utasa.

2.Ni namba ya kuharibu vizuizi.
Vipo vizuizi kwenye maisha yako, ambavyo vimesimama nawe unashindwa kupita, 2017 ni mwaka kiunabii maana yake hauzuiliki, hakuna uchawi utaweza, hakuna uganga utajaribu, ni mwaka wakutozuilika.
Yoshua 6: 1-27
Wana waisraeli walipovuka mto yorodani, walizuilika walipofika yeriko, kuta zilijengwa kwaajili ya wana waisraeli ili wasiimiliki nchi ya ahadi, kihistoria wanasema kuta za yeriko upana wake zingeweza kupitisha gari nne basi kubwa kwa wakati mmoja. Lakini Mungu akamwambia Yoshua waambie makuhani saba watangulie mbele, na watu wote wauzunguke ukuta wa Yeriko siku sita na siku ya saba wazunguke mara saba kisha washangilie na kupiga kelele kuta zitaanguka, hili lilikuwa ni tendo la kinabii la Kimungu lililokamilishwa katika namba saba, kweli wana waisrael walifanya kama Mungu alivyowaambia, kuta za yeriko zikaanguka mwaka 2017 huo ukuta ambao umesimaa kwenye maisha yako unabomoka kwa jina la Yesu, haijarishi niwakina nani wanaosimamia huo ukuta,Najua unayesoma hizi habari ni kama hadidhi kwako lakini nakwambia ipo neema 2017, utaomba kazi, utapewa bila kuzuilika maana kupo kukamilishwa katika namba saba.

3.Ni namba ya kumkumbusha Mungu agano alilofanya na watu wake.
Watu wengi wanasema Mungu amenisahau, mbona ni kama hayuko, ila mwaka 2017 Mungu anawakumbuka watu wake tena.
Mwanzo 9:13
Mungu alipogharikisha kile kizazi kwa mvua, nyakati za Nuhu, baada ya dhambi zao kuzidi mbele za Mungu, Mungu hakusaza uovu uendelee juu ya nchi, bali alimwacha Nuhu mwenye haki wake, baada ya Nuhu kutoka ndani ya safina Mungu akamwambia Nuhu sitoipiga tena dunia kwa mvua, naweka igano kati yangu na kila chenye mwili, Mungu akatokeza upinde wa mvua katika anga akasema upinde huu wa mvua ni ishara ya agano kati yangu na kila chenye mwili kwamba sitaipiga tena dunia kwa mvua.
Upinde wa mvua ni rangi saba, maana yake namba saba, katika namba saba Mungu amehaidi apigi tena dunia, ndiyo maana upinde wa mvua hutokea kila kipindi cha mvua maana yake Mungu anataka kuipiga dunia ila anaghairi kwa upinde wa mvua kutokea, maana upinde wa mvua umebeba kumbukumbu, juu ya maisha ya watu.
 Yapo mengi Mungu uliagana naye yataenda kutokea 2017, maana ni namba ya unabii huruma za Mungu zinasimama kukutetea.

4.Ni namba ya watoto wa Mungu kumiliki.
Mungu anataka umiliki, wewe usiyenacho 2017 siyo namba ya kawaida kiunabii maana ni saba imesimama, ukiwa mtoto wa Mungu utamiliki vitu vikubwa, utamiliki pesa za kutosha, kwasababu ni mwaka wa kumiliki.
Ufunuo 11:15.
Malaika wa saba akapiga baragumu pakawa na sauti kuu, katika mbingu, zikisema ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana Mungu wetu na wa Kristo wake na atamiliki milele na milele.

Malaika wa saba, alipopiga baragumu ya saba, utawala wa Kimungu ukaanza duniani, ufalme wa Mungu ukaanza kumiliki juu ya nchi.Maana ya ufalme wa Mungu kumiliki duniani maana yake vitu vinavyoendelea mbinguni vitaendelea na duniani, kama mbinguni hakuna umasikini maana yake duniani pia umaskini utaondolewa, kama mbinguni hakuna magonjwa maana yake duniani watu watafunguliwa dhidi ya magonjwa maana ikisoma saba watoto wa Mungu wanamiliki, waza makubwa wala siyo madogo, 2017 ni muda wa kuwa juu kiuchumi, maana ufalme wa Mungu umejiimalisha kiuchumi.

5.Ni namba ya kuponywa magojwa.
Mwaka 2017 yaambie magonjwa bye bye, maana siyo mwaka wa kawaida kiunabii mahali popote iliposoma saba magonjwa sugu yaliyoshindikanika, yasiyo na dawa Mungu anaachilia uponyaji haijarishi umekaa hospitalini kwa muda gani, au madaktari wamzungumza nini tembea mwaka 2017 katika uzima kwa jina la Yesu.

2wafalme 5:1-19.
Naamani mkuu wa jeshi la shami alimwendea nabii Elisha ili amponye ukoma wake, nabii Elisha akamwambia nenda kajichovye mara saba kwenye mto Yorodani utapona ukoma wako, Naamani alipojichovya mara saba ukoma wake ukatakasika naye akawa mzima tangu saa ile. Mwaka 2017 ni namba ya unabii, ni namba ambayo wewe mtoto wa Mungu utaondoka kabisa katika ugonjwa wako.

Kumbuka mtu aliyeokoka haishi kwa uzowefu bali kwa ufunuo wa Mungu, tembea katika neema ya Mungu 2017,

MAMBO YA KUFANYA 2017.
Hakikisha kila unapokutana na tatizo unalicheka kwamba limekosea njia, mwaka wako wa kumiliki, Endelea kukili kwa kinywa chako kila kilichoambatanisha 2017.


NEEMA ILIYOPO 2017 NEEMA ILIYOPO 2017 Reviewed by adam on Desemba 31, 2016 Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.