NEWS

Kujiweka mahali pamfalme



      
Kuna mahali Mungu amekuweka, wewe usipojiweka kuna vitu utashindwa kupokea kutoka kwa Mungu.Yapo mabadiliko ndani yako kama utajiweka mahali pamfalme maana mahali pafalme ndipo Mungu amekuweka.Mungu anataka utoke kwenye taabu ulizonazo hivyo inakupasa kujiweka mahali pamfalme, Mwanafunzi asipojiweka mahali pa uanafunzi hawezi akajifunza, ukijiweka mahali pamfalme utavaa kama mfalme, utakula kama mfalme, na utazungumza kama mfalme.



Kuna namna ambavyo Mungu anataka alione kanisa lake linaishi leo, mfano ukienda Benki leo ukachunguza watu waliopo hapo utajua huyu ni muudum na huyu ni mteja kutokana na mahali walipojiweka, Ukiona leo mtu ameshika jembe anaenda shambani utajua kwamba huyu ni mkulima, kwasababu amejiweka mahali pamkulima, ili uishi kifalme itategemeana umejiweka mahali pamfalme.
Kuna baraka leo zinakupita kwasababu ujajiweka mahali pamfalme, unaweza ukadharaulika kwasababu ya mahali ulipojiweka.
                                                        Isaya  9:6
Kwa maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, nao uweza utakuwa begani mwake.  Naye ataitwa: Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.

Huyo mtoto atakayezaliwa uweza wakifalme utakuwa begani mwake, uweza wa kifalme hautakuwa kichwani pake, uweza wakifalme utakaa  begani mwake maana yake mamlaka ya kifalme itakaa kwenye mabega yake.
                                                    Kolosai 1:18.
Yeye ndiye kichwa cha mwili, yaani, Kanisa, naye ni wa mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ili Yeye awe mkuu katika vitu vyote

Huyo mtoto ndiye kichwa cha mwili yaani cha kanisa
Huyo mtoto atakayezaliwa yeye ni kichwa na mabega yake ni mwili wake, mwili huanzia kwenye mabega, mabega yake ndiyo mwili wake, mwili wake ndiyo kanisa kwa hiyo anaposema mamlaka ya kifalme itakuwa begani pake maana yake itakuwa mwilini mwake maana yake mamlaka yakifalme itakaa kwa kanisa na kanisa ni wewe.
Wewe ndiye unayeitumia hiyo mamlaka ya kifalme, wewe ndiye mabega ya Yesu mamlaka ya kifalme ipo kwako maana wewe ni mwili wa Yesu.
 


                                            KWELI MBILI KUHUSU MAMLAKA YA KIFALME
1.Mfalme anatawala anaongoza kwa neno lake.
 

Muhubiri 8:4
Kwa kuwa neno la mfalme lina nguvu, nani awezaye
kumwambia, “Je, wewe unafanya nini?’

Ukijiweka mahali pamfalme neno lako lina nguvu, Ukiongea wewe unakuwa kama Alfa na Omega katika mamlaka yako.
Kwahiyo mtu aliyejiweka mahali pamfalme kila anachokisema kiwe kibaya au kizuri kinatokea, mfalme sikuzote ndiye mwamuzi wa mwisho ukijiweka mahali pamfalme utakuwa mwamuzi wa mwisho.
Kwa neno lako unaweza ukafunga na ukafungua, kwa neno lako unaweza ukauwa na uakahuisha, Neno lako linaweza likabadilisha mazingira.
Yusuphu anaambiwa na mfalme atolewe gerezani na aletwe ikulu, kwa neno la mfalme mazingira ya mfalme yalibadilika.

Zaburi 105:20
Mfalme alituma akamfungua,mtawala wa watu alimwachia huru.

2. Kila kitu kipo chini ya miguu yake.


 
1wakorintho 15:27
Kwa maana Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu
yake.” Lakini isemapo kwamba, ‘‘Vitu vyote
vimewekwa chini Yake,” ni wazi kwamba Mungu
aliyetiisha vitu vyote chini ya Kristo hayumo
miongoni mwa hivyo vilivyotiishwa`

Kila kitu Mungu amekiweka chini ya miguu yake Yesu, yeye Yesu ni kichwa na kanisa ni mwili, miguu ni sehemu ya mwili,na mwili wa Kristo ni wewe, kwa hiyo kila kitu Mungu amekiweka chini ya kanisa, kila unachokitaka kipo chini yako haijarishi ni kitu gani. Unapojiweka mahali pamfalme unakuwa si mtu wa kawaida kila kitu kipo chini yako, kama vile raisi wa nchi alivyo ndivyo ulivyo kila kitu kipo chini yako, kazi yako ni kuagiza na utendaji kazi utatokea maana unalo jopokubwa la malaika linatembea na wewe.


Jiweke mahali pamfalme, maana Mungu anataka akuhamishe viwango, akutoe mahali ulipo akuweke mahali pengine, ni kazi kwako kujitambua na kutembea na mamlaka ya kifalme.









      


Kujiweka mahali pamfalme Kujiweka mahali pamfalme Reviewed by adam on Januari 16, 2017 Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.