Kwanza lazima ujue kuwaombea viongozi ni agizo la Mungu, ili viongozi wa nchi waiongoze nchi vizuri wanahitaji serekali ya mbinguni iwasaidie kuongoza nchi.
1Timotheo 2:1-2
Basi kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala na maombezi, na shukrani zifanyike kwaajili ya watu wote.Kwaajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani.
Mungu ameona magonjwa, na vita kubwa wallionayo viongozi wa nchi ameona watu wanaishia kulalamika si kuomba, wanaishia kuwasema vibaya si kuwafanyia dua na maombezi, Mungu anatoa suluhu kwetu Watanzania kwamba tuombe kwaajili yao, ili tuishi maisha ya utulivu na amani, kumbe vingozi wa nchi ndiyo wanaoweza wakaharibu amani ya nchi, au wakaitengeneza, hivyo sisi kama watanzania tusipochukua nafasi katika kuwaombea tutaishia kuwasema ila wasibadilike.
Ni jambo la kusikitisha kwamba eti hata wakristo nao wapo kwenye makundi makundi ya kumponda Raisi wa nchi katika vijiwe wamesahau agizo la Mungu, kwamba mkristo hajaruhusiwa kumsema vibaya Raisi wake ila kumwombea.
Yeremia.29:7
Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa Bwana kwamaana katika amani ya mji huo ninyi mtapata amani.
Ni mara ngapi umefanya maombi kwaajili ya Raisi wako wa nchi ?, au ni mara ngapi umenungunika na kumsema vibaya ? utasema sana juu ya raisi wako magufuli lakini hatobadilika, mpka pale tu utakapo anza kuomba kwa ajili yake.
Wakati mmoja Petro alikamatwa na kiongozi wa nchi, mfalme Herode, akawekwa ili alindwe ndani ya gereza, ili baada ya pasaka kisha atundikwe anyongwe, lakini kanisa liliposikia kwamba Petro amekamatwa liliingia kumwomba Mungu, ili Mungu amfungue kwenye hili gereza baada ya maombi Mungu akatuma malaika kwenda kumfungua Petro Gerezani na Petro akatoka akiwa salama kabisa. Matendo 12.
Iga mfano wa kanisa la kwanza, wao hawakuingia kugombana na kongozi wao bali kumwomba Mungu, walitaji serekali ya mbinguni iwasaidie duniani, inaezekana kwa namna moja ama nyingine unamwona Raisi wa nchi ni kama kafunguia uchumi wako kwenye gereza wewe omba tu kwa Mungu baada ya maombi yako Mungu atatuma malaika kuongea na huyo kiongozi wa nchi naye atachilia mali zako.

MWOMBEE RAISI MAGUFULI USIMSEME VIBAYA
Reviewed by adam
on
Aprili 07, 2017
Rating:
![MWOMBEE RAISI MAGUFULI USIMSEME VIBAYA](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEifggxiRF2e53r1T9GCihHCk0a0br3ES2tzOrqdfl1I98OMpav_fbF50HM5GOLzHBJp07vBys3wQQKArnXhjeQHc_uCn2arRVEOLxEuSd8zHGj5Ts_WJHr2YDQdNNJVWfkvyHs4Tguto0gZ/s72-c/index.jpg)
Hakuna maoni: