![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3yfZQPFl2pPRIhnTKCPiFaUNtAzM-S9Y-xz8DxY55y1IC-9R59nyIg4MRa4uws2PplnyJ6m0yDk4_lB7uXSu23l4549kLmBDGfICJBr3n9h89t-Yl2GHbE7o3m2k9b6YR4YTqeD828-95/s1600/15219384_829068300567464_6240384121028183468_n.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgCD3_qcWnDRXxU6TXwLeOc6686d9mN0s4tnOQPdn9pGZ3w7izD8gf0tAXbKPPx61KgGiL0-JL3aTkPiQFk9TYAa_HfZK_Tvz5X0al8kSTS_G4o4UbTeXVG4Dp41VnF8icYzZXPHBp3HuYc/s1600/index3.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZ5JjvnpqjHe63chYLstOPBuKmb2NF6h8tWB4eVNS-LOSQAljLucD7MB061c_nCOfvFYYt-QBrem5SyHNTsOjvlbPGz12-Dd0RmH3mtwSPSjXzpoz0R9HGF265Yj1In9AeGpBHcI-q0B2J/s1600/images1.jpg)
Kupamiliki maana yake kupaweka chini yako, pawe katika amri ya kinywa chako, Upaendeshe si wewe pakuendeshe.
Ulipopewa na Bwana panaweza kukuendesha pale tu usipoitambua mamlaka yako.
Unaweza ukawa mwanajeshi mwenye siraha, lakini haujui kuitumia siraha yako, hivyo utamilikiwa na mahali pale ambapo ukitakiwa upamiliki wewe.
Pia unaweza ukawa unafunguo za gari unalolimiliki wewe lakini haujui namna ya kuliendesha.
Hiyo mamlaka uliyopewa juu mahali fulani ni kukamilisha kusudi la Mungu
Yoshua 1:3
Kila mahali zitakapokanyaga nyao za miguu yako nimekupa.
1.Ina maana hii mamlaka ya sehemu fulani(mtaa, kijiji,kata,tarafa,wilaya, mkoa,nchi)imebebwa na mtu fulani aliyekabiziwa mahali hapo.
Mamlaka ya nchi ya Tanzania imebebwa na Raisi wa Tanzania aliyekabiziwa Tanzania.
Mamlaka ya chuo fulani imebebwa na mkuu wa hicho chuo aliyekabithiwa hilo eneo,
ikiwa inamaana hii hakuna kitu kuingia wala kutoka pasipo raisi wa nchi ya Tanzania.
Nikiwa nina maana hii kama Mungu amekupa ofisi fulani au eneo fulani, usiruhusu kitu fulani kakaendelea bila wewe kujua au kuruhusu
2.Mungu anamaana hii hautobadilishwa na mamlaka uliyoikuta uliyoikuta mahali hapo, Bali upo hapo ili kubadilisha hiyo mamlaka.
Akiwa na maana hii hiyo hali ya hewa utakayoikuta mahali hapo haitokubadilisha wewe bali wewe utaibadilisha, maana imewekwa chini ya miguu yako.
Daniel 3:28e-29.
Wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao wasimtumikie
Mungu Mwingine wala kumwabudu ila Mungu wao.
Maandiko yanaposema waligoma kuabudu sanamu ya mfalme, maana yake walikataa kumilikiwa na ufalme wa babeli, wana waisraeli walipomilikiwa na eneo fulani walikuwa wakijihusisha na sanamu za hilo eneo.
Mfalme Nebokadreza hakuchukia tu kwasababu wamegoma kuabudu sanamu bali wamegoma kumiliwa na mamlaka ya babeli.
Kwasababu walikuwa wanamilikiwa na ufalme wa babeli kitu cha kwanza mfalme kuwasimamishia ni sanamu, kama hutokubali kulimilki eneo unalolikanyaga zitasimama sanamu kwenye maisha yako.
Shadraki, Meshaki na Abednego walipopamiliki walipopakanyaga wakabadili neno la mmiliki wao.
Maana yake walikuta Rushwa wao wakageuza kuwa ukweli, walikuta magonjwa wao wakageuza Afya, walikuta laana wao wakageuza Baraka.
Eneo ulilopo umepewa na Mungu, kuwepo kwako hapo si kwa bahati mbaya Mungu anataka afanye kitu kwa utawala wako elewa mamlaka yako na utembee katika hiyo mamlaka.
![Kupamiliki ulipopewa na Bwana](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3yfZQPFl2pPRIhnTKCPiFaUNtAzM-S9Y-xz8DxY55y1IC-9R59nyIg4MRa4uws2PplnyJ6m0yDk4_lB7uXSu23l4549kLmBDGfICJBr3n9h89t-Yl2GHbE7o3m2k9b6YR4YTqeD828-95/s72-c/15219384_829068300567464_6240384121028183468_n.jpg)
Hakuna maoni: